Posts

Showing posts from 2012

WANYAMA NA TABIA ZA BINADAMU

Image
Habari zenu ndugu wapenzi wa Hekimastories, Leo nimeamua kuleta kitu kingine tofauti na stori kama tulivozoea, katika soma soma vitabu mbalimbali nilipata kitu amabacho nilipenda kukileta hapa kwenye blog ili niweze kugawana maarifa na ndugu zangu popote pale mlipo. Dunia imeumbwa na vivutio vingi sana, vingi vizuri na vinapendeza, ikiwemo Milima, Mito, Bahari, Wanyama, Misitu na vingine vingi siwezi vimaliza. Lakini hivi vitu ijapokua ni vizuri kwa kuvitazama lakini pia vinamafunzo makubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku kama ukivichunguza kiundani. Hivyo basi ningependa kukupa fursa hii kutulia japo kwa dakika tano tu, chagua kitu chochote kile unachokipenda katika dunia hii, tuliza mawazo yako, kua mtulivu iweke picha ya iko kitu ndani ya mwili wako alafu fikiri kwa utulivu inakueleza nini katika maisha yako ya kila siku. Ni zoezi fupi lakini kama utakua ukifanya kila siku utaona jinsi mambo yako yatakavyo kuwa marahisi na kunyooka. Mimi leo nilitaka tujadili kuhusu  t...