NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE?
Kulikuwa na duka Kuubwa la Vyakula na Vinywaji katika
mji. Panya Wengi waliishi katika duka
hilo la vyakula na vinywaji. Chakula kilikuwa ni kingi sana kwa ajili yao. Walikula
kila kitu na kuharibu mifuko yote ya vyakula. Waliharibu pia mikate, biskuti
na matunda ya duka.
Mwenye duka alishikwa na wasiwasi kweli. Hivyo, yeye alipata
wazo "mimi lazima ninunue paka na atakaa humu ndani ya hili duka. Kufanya
hivo naweza kuokoa mambo yangu."
Alimnunua Paka mmoja mzuri, mkubwa na kisha kumwacha
pale. Paka alikuwa na wakati mzuri wa kuwinda panya na kuwaua. Panya hawakuweza
kuzunguka kwa uhuru sasa. Waliogopa kwamba wakati wowote paka ange wakamata na kuwala.
Panya walitaka kufanya kitu fulani. Wakaitisha mkutano na
wote wakasema "Ni lazima kujikwamua na paka. Je, kuna mtu ana maoni?"
Panya wote wameketi na kuogopa. panya mmoja mwelevu alisimama
na akasema, "paka hatembea kwa upole. Hilo ni tatizo. Kama tunaweza kumfunga
kengele kwenye shingo yake, basi mambo yatakuwa mazuri. Tunaweza kujua harakati
zake zote ".
"Ndiyo, hilo ni jibu sahihi," walisema
panya wote. panya wa miaka mingi alisimama polepole na akauliza, "Ni Nani atakaye
Mfunga paka kengele? " Baada ya muda mchache hakukuwa na yeyote wa kujibu
swali hili.
Hekima:
Ufumbuzi Mtupu hauna
thamani.|Hekima stories
Comments