Posts

Showing posts from May, 2018

MUONGO HAAMINIKI HATA AKISEMA UKWELI

Kulikuwa na kijana mmoja akichunga Kondoo wa kijiji juu ya kilima. Yule Kijana akajilaza juu ya kilima hiko akiwa amechoka na kuboreka   baada ya kuchunga wale kondoo kwa muda mrefu siku hiyo.  H ivyo akafikiria kufanya kitu kitakacho mchangamsha.   Akavuta pumzi   kuubwa na kupiga kelele, “Simba! Simba! Simba!   Huku akiwafukuza wale kondoo. Wanakijiji walikuja wakikimbia juu ya kilima ili kumsaidia yule kijana. Lakini walipofika juu, hawakukuta simba.   Yule kijana aliwacheka mbele ya nyuso zao zilizo jaa hasira. Wale wanakijiji wakamwambia yule kujana "Usipige kelele za Simba wakati hakuna Simba !", Wakashuka chini ya mlima huku wamekasirika. Baadaye, kijana huyo alipiga kelele za simba tena, "Simba! Simba anakimbiza kondoo!” Kwa furaha yake mbaya, aliwaangalia wanakijiji wakipanda tena kile kilima ili kumsaidia kufukuza Simba. Wanakijiji walipofika juu pasi na kuona Simba, wakasema kwa ukali, "Piga kelele za kuomba msaada wakati kuna kitu ch...