MUONGO HAAMINIKI HATA AKISEMA UKWELI
Kulikuwa na kijana mmoja akichunga Kondoo wa kijiji juu ya kilima. Yule Kijana akajilaza juu ya kilima hiko akiwa amechoka na kuboreka baada ya kuchunga wale kondoo kwa muda mrefu
siku hiyo. Hivyo akafikiria kufanya kitu
kitakacho mchangamsha.
Akavuta pumzi kuubwa
na kupiga kelele, “Simba! Simba! Simba!
Huku akiwafukuza wale kondoo.
Wanakijiji walikuja wakikimbia juu ya kilima ili kumsaidia
yule kijana. Lakini walipofika juu, hawakukuta simba. Yule kijana aliwacheka mbele ya nyuso zao
zilizo jaa hasira.
Wale wanakijiji wakamwambia yule kujana "Usipige kelele
za Simba wakati hakuna Simba !", Wakashuka chini ya mlima huku
wamekasirika.
Baadaye, kijana huyo alipiga kelele za simba tena,
"Simba! Simba anakimbiza kondoo!” Kwa furaha yake mbaya, aliwaangalia
wanakijiji wakipanda tena kile kilima ili kumsaidia kufukuza Simba.
Wanakijiji walipofika juu pasi na kuona Simba, wakasema kwa
ukali, "Piga kelele za kuomba msaada wakati kuna kitu cha Hatari kweli!
Usipige kelele za ‘Simba’ wakati hakuna Simba!"
Lakini Yule mvulana alidharau na kucheka wakati wanakijiji
wakishuka chini ya kilima kwa hasira.
Baadaye, aliona Simba wa kweli akinyemelea Kundi la kondoo
kule kilimani. Yule kijana
alichanganyikiwa na kuanza kupiga kelele kwa nguvu na sauti kubwa kuliko awali,
“Simba! Simba! Simba!”
Lakini wanakijiji walidhani alikuwa anajaribu kuwadanganya
tena, na hivyo hawakuenda kutoa msaada.
Jua lilipozama, kila mtu alijiuliza kwa nini mvulana huyo
mchungaji hakurudi kijiji na kondoo wao. Walipanda kilima ili kumtafuta.
Hatimae wakamkuta akilia.
"Simba alikuja hapa kweli! Kondoo
wote wametawanyika!" Nililia, "Simba!" Kwa nini humkuja
kunisaidia? "
Mzee mmoja alijaribu kumfariji yule
kijana wakati wanaludi kijijini.
"Tutakusaidia kutafuta kondoo
waliopotea kesho asubuhi," alimwambia, uku akizungusha mkono wake juu ya
bega la yule kijana, "Hakuna mtu anayemuamini mwongo .. hata pale
anaposema ukweli!"
Comments