Posts

Showing posts from 2019

HAKUNA KAMA MAMA

Baada ya kumaliza Masomo yake, aliamua kuaga wazazi wake na kwenda Mjini kutafuta maisha. Alipofika mjini aliajiriwa kwenye kampuni ya Wachina, malipo ya mshahara wake yalikuwa madogo sana hayakuweza kukidhi mahitaji yake ya mwezi, ilikuwa ikifika katikati ya mwezi hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa inakosekana. Lakini alijitahidi kujinyima, kidogo alichokipata alikuwa akihifadhi na kila alipokuwa akiwatembelea wazazi wake alikuwa anawapelekea pesa kidogo na kuludi mjini kuendelea na maisha yake. Yule kijana alijiwekea malengo baada ya miaka mitatu aweze kuwa na mtaji wa kufanya biashara itakayo ongeza kipato   mbali na kile cha kuajiriwa.   Kila alipokuwa akimpigia simu Mama yake, cha kwanza alikuwa akiulizwa maendeleo ya mipango hiyo.   Majibu hayakuwa mazuri. Hakuna alichokuwa anakibakisha kila mwezi, ilikuwa ni ngumu kutokana maisha ya mjini, ila pamoja na hayo yote alikuwa lazima akawaone wazazi wake na kumwachia mama yake kiasi cha pesa kwa ajili ya matumizi ...