HAKUNA KAMA MAMA
Baada ya
kumaliza Masomo yake, aliamua kuaga wazazi wake na kwenda Mjini kutafuta
maisha.
Alipofika
mjini aliajiriwa kwenye kampuni ya Wachina, malipo ya mshahara wake yalikuwa
madogo sana hayakuweza kukidhi mahitaji yake ya mwezi, ilikuwa ikifika katikati
ya mwezi hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa inakosekana. Lakini alijitahidi
kujinyima, kidogo alichokipata alikuwa akihifadhi na kila alipokuwa
akiwatembelea wazazi wake alikuwa anawapelekea pesa kidogo na kuludi mjini kuendelea
na maisha yake.
Yule
kijana alijiwekea malengo baada ya miaka mitatu aweze kuwa na mtaji wa kufanya
biashara itakayo ongeza kipato mbali na kile
cha kuajiriwa. Kila alipokuwa akimpigia
simu Mama yake, cha kwanza alikuwa akiulizwa maendeleo ya mipango hiyo. Majibu hayakuwa mazuri. Hakuna alichokuwa
anakibakisha kila mwezi, ilikuwa ni ngumu kutokana maisha ya mjini, ila pamoja
na hayo yote alikuwa lazima akawaone wazazi wake na kumwachia mama yake kiasi
cha pesa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Baada ya
Miaka Mitatu, yule kijana hakuweza kutimiza
malengo yake. Alienda kuwatembelea wazazi wake kama kawaida yake. Katikati ya
Maongezi yao, Mama yake akamuuliza maendeleo yake pamoja na Mipango ya biashara
aliyotaka kuifanya. Majibu yake yalikuwa yakukata tamaa na alipanga kutafuta
kazi nyingine yenye kipato kikubwa zaidi ya anachopata kwa sasa.
Mama
yake, akamwambia subili niingie ndani kuna ujumbe wako nikupe. Mama akaingia
ndani na kutoka na Kiasi cha Pesa alichokuwa akihitaji kwa ajili ya biashara
yake.
Yule kijana alipigwa butwaa, akamuuliza mama yake, “mama umepata wapi pesa zote
hizi? na hali ya maisha yako binafsi sio nzuri, hadi mimi nikuletee pesa kutoka mjini.”
Mama akamjibu, “ulipokuwa
unaniambia hali ya maisha yako sio nzuri kutokana na kipato chako, pesa zote
ulizokuwa unaniletea nilikuwa nakuhifadhia mwanangu, sikuwahi kutumia hata kidogo, najua
una moyo wa kutusaidia na kututunza wazazi wako lakini mafanikio yako ni furaha
kwetu wazazi wako"
Comments