MZEE MWENYE HEKIMA NA BUSARA
Hapo zamani kulikuwa na Mzee mmoja mwenye busara sana, alikuwa akiishi kwenye kijiji kimoja huko nchini Korea. Aliishi maisha ya tabu sana, ambapo aliweza kujifunza sana kutokana na maisha hayo, alikuwa akitumia akili nyingi na kufikiri kwa kina sana kutatua changamoto zilizokua zikimkuta. Watu kutoka sehemu mbalimbali walimfuata na kumuomba ushauri juu ya matatizo yao. Alikuwa akisikiliza kwa umakini na unyenyekevu mkubwa sana na hata alipokuwa akitoa ushauri alikua akitoa kwa umakini na hekima pia. Hii ilifanya watu wengi zaidi kumfuata kutoka sehemu za mbali sana kuja kuwa karibu na kuzungumza nae. Kulikuwa na Kijana mmoja pale kijijini, aliwashangaa watu wanaosafiri kwenda kuzungumza na huyo Mzee, “Anaujuzi ganu huyo mzee?” alikua akisema huyo kijana. “Hakusoma hata dirasa moja, na siamini kama anahekima kiasi gani watu wamfuate!” pindi akijiuliza kichwani kwake akapata wazo la kwenda kujaribu hiyo hekima ya yule mzee. Yule Kijana alikwenda porini na kukamata ndege mdogo, alafu...