MAMA NA MBWA

Katika kijiji fulani Kulikua na mama mmoja alikua akiishi na Mtoto na Mbwa mmoja mweupe mzuri sana. Yule mama alikua akitoka pale kijijini kwenda safari ndefu kutafuta riziki yake na mtoto wake mdogo.
Pindi alipokua akitoka nyumbani alikua akimuacha mtoto wake na mbwa akimlinda mtoto huyo na mzingira ya kila kitu ya pale nyumbani hadi anapoludi.
Siku moja yule mama alimuacha mtoto wake nje na kwenda sokoni mara moja. Alipoludi alimkuta mbwa wake ameloa damu na zingine zikivuja kwenye kucha na mdomoni.Yule mama alikimbia kumuangalia kama mtoto wake yupo salama pale alipomueka, akakuta kulikua na purukushani na damu zimedondoka na mtoto wake hayupo. Alilia sana yule mama na akachukua fimbo moja kubwa sana kwenda kumpiga yule Mbwa hadi kufa.
Wakati akiludi ndani baada ya hilo tukio alimkuta mtoto wake chini ya kitanda akiwa salama kabisa na pembeni yake kulikua na mnyama mkali amekufa akiwa na majeraha.

Hii ni hadithi fupi, lakini inaujumbe mzito sana katika maisha ya kila siku. Wangapi wanaweza kujifananisha kama huyu mama, wangapi wamekua wakifanyiwa kama huyu mbwa.? Ni mara ngapi tumekua tukifanya maamuzi bila subira, bila ya kuchunguza kwanza? Ama tumewahi kuwa na shukurani kwa wale wanaotusaidia kila siku, tazama wema wote wa yule mbwa kulinda nyumba na yule mtoto, mwisho wake anauwa kwa kosa la siku moja tu.

kuna mengi sana tunaweza kuyapata kwenye hii stori, hayo ni ya kwangu nilipenda niwape lakini mengine mengi tunaweza kuyapata kutoka kwako! Fikilia kwa makini zaidi, angalia pia ni jinsi gani tunavyoishi kama huyu mama mwenye Mbwa mzuri.

Comments

Popular posts from this blog

NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE?

WANYAMA NA TABIA ZA BINADAMU