WANYAMA NA TABIA ZA BINADAMU

Habari zenu ndugu wapenzi wa Hekimastories, Leo nimeamua kuleta kitu kingine tofauti na stori kama tulivozoea, katika soma soma vitabu mbalimbali nilipata kitu amabacho nilipenda kukileta hapa kwenye blog ili niweze kugawana maarifa na ndugu zangu popote pale mlipo.

Dunia imeumbwa na vivutio vingi sana, vingi vizuri na vinapendeza, ikiwemo Milima, Mito, Bahari, Wanyama, Misitu na vingine vingi siwezi vimaliza. Lakini hivi vitu ijapokua ni vizuri kwa kuvitazama lakini pia vinamafunzo makubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku kama ukivichunguza kiundani. Hivyo basi ningependa kukupa fursa hii kutulia japo kwa dakika tano tu, chagua kitu chochote kile unachokipenda katika dunia hii, tuliza mawazo yako, kua mtulivu iweke picha ya iko kitu ndani ya mwili wako alafu fikiri kwa utulivu inakueleza nini katika maisha yako ya kila siku.
Ni zoezi fupi lakini kama utakua ukifanya kila siku utaona jinsi mambo yako yatakavyo kuwa marahisi na kunyooka.

Mimi leo nilitaka tujadili kuhusu  tabia zetu Binaadamu kwa kulinganisha na tabia za Wanyama. na jinsi tabia zinavyoharibu maendeleo katika jamii zetu, kama vile familia, vikundi vidogo vyenye lengo fulani zuri tu la maendeleo. Tabia ni kama ngozi huwa ni ngumu kubadilika, mara nyingi tumekua tukiwakimbia watu wenye tabia tofauti na tulizo nazo, tunashindwa kufanya kazi nao kwasababu hatufanani tabia zetu matokeo yake malengo yetu yanavunjika.

Kulikua na Kikundi kimoja katika kijiji cha Mkuranga, kilikua kuna Mwenyekiti na viongozi wote wanaopasa kuwepo katika kikundi, lakini Mwenyekiti alikua ni mkali sana, hakupenda mambo yaende tofauti na makubaliano ya kikundi, lakini ndai yake kulikua na wanachama ambao hata kama anamawazo mazuli hapeleki kwenye kikundi wakimuogopa Mwenyekiti, wengine walikua wakisambaza maneno pembeni wanasema kiongozi huyo ana masrahi binafsi katika kikundi hivo wakasababisha kundi lote kupolomoka, wengine waliomba kuludishiwa pesa zao za hisa, kulikua na mazao yalipandwa kwa pamoja, wakang'oa na kugawana mali za kikundi.  

Huu ni mfano mdogo wa kikundi, ipo mingine mingi sana. Fikiri ni familia ngapi amabazo zinasambalatika kwa sababu Mama au baba ni mkali? watoto hawapati fursa ya kusema au kufanya chochote kwenye familia, mtoto akisikia mngurumo wa  gari tu nje, kama aliwasha friji, ama video anazima haraka haraka ili asije pigwa anamaliza umeme, watoto hawapati fursa ya kuongea wanapo hitaji msaada kwa wazazi. Hii ipo hata kwa watoto pia, Mtoto mwingine ankua na tabia ambayo wazazi wanaomba shule zisifungwe, maana akiludi nyumbani yeye ndiye anakua kama mwenye familia, ubabe ubabe ndani ya nyumba.

Hatuwezi kuendelea kama tusipofahamu tabia za kila mtu anaye tuhusu, tupate muda mzuri kutambuana, Fahamu Mwenyekiti, Baba, Mama, ama mtoto anatabia gani, wewe binafsi jitambue unatabia gani, toa Mrejesho kwa Mtu anayekukwaza kwa kutumia Kauli Mimi.."I statements" Toa fursa kwa kila mtu akueleze unavyoishi na watu, usipinge utakachoambiwa kwasababu watu wanaokuzunguka ndio wanaokufahamu vizuri kushinda wewe mwenyewe kisha fanyia kazi hiyo mirejeshoo utakayo ipokea, hivyo utaona mabadiliko yako binafsi pamoja na jamii yako. Inafahamika kuwa ni ngumu sana kubadili tabia ya mtu lakini inawezekana kama ukifanyia kazi japokua itachukua muda mrefu.

Wafuatao ni baadhi tu ya Wanyama na tabia zao, ambazo Mimi, wewe tunazo na wakti mwingine ni vikwazo kwa watu wanaotuzunguka.

1. PUNDA:  anaposema "Siendi" haendi hata umpige na gogo la mbuyu. kuna watu ambao waking'ang'ania wazo moja hata aambiwe ukweli aje, habadilishi wazo lake.
PUNDA

2:  SIMBA: Huyu ni mgomvi" watu wenye tabia za simba wapo tayari kupigana kwa vyovyote vile na yeyote yule anayeingilia mipango ama matakwa yao.                                                                                   
SIMBA
 3: SUNGURA: yeye ni kutimua Mbio tu. Watu wenye tabia ya Sungura siku zote hawatatui tatizo, wakiona ugomvi ama vuguvugu la ugomvi linataka kutokea haraka sana wanabadilisha maada. Hawa ni waoga
SUNGURA
Leo nimejalibu kuweka hao wachache, ila wapo wengi jalibu kutembelea kila siku Blog hii utapata kuona jinsi tabia zetu zinavyofanana na wanyama. Leo unaweza usione tabia unayofanana nayo ila nakuhaidi posti ijayo utaikuta.       


4: NYANI:  Anapumbaza na Mcheshi,   Mara nyingi watu wenye tabia za nyani huwa wanapenda kuwa wachekeshaji sana na wanapumbaza  wenzao pale wanapokua wanafanya mambo muhimu.

NYANI
5: NYOKA: Huyu huwa anapenda kujificha kwenye nyasi na huruka ghafla na kung'ata. Wapo watu wenye tabia kama za nyoka, Mara nyingi huwa wanakaa kimya kwa muda mrefu wakati jamii fulani ikiwa inashiriki kufanya jambo, lakini endapo wakisema jambo moja tu huaribu kila kitu kinachoendelea.

NYOKA

6: KOBE: Huyu upenda kujiingiza ndani ya nyumba yake endapo mazingira hayapo shwari, na hujitoa anapohisi hali imekua shwari nje. Wapo watu watabia kama za kobe, hupenda kujitoa kwenye jamii ama kundi endapo kuna matatizo, hawatoi mchango wowote ule, kama wa mawazo, pengine wangependa jamii isifahamu kama wapo ndani ya hiyo jamii ili wasisumbuliwe kabisa.

KOBE
7: TEMBO: Anatabia ya kuangusha miti barabarani, na kuzui njia ili chochote kisipite hadi atakapo amua yeye. Wapo Ndugu zetu wenye hizi tabia, wanakua wasumbumbufu, wababe huzuia kundi kuendelea na shuguli zake kufikia malengo yaliyopangwa.


TEMBO
8: MBUNI: Huona kila kitu kipo sawa wakati wote, hawafikiri kama kuna tatizo kamwe. Wapo watu wenye tabia kama za Mbuni, mara nyingi huinamisha kichwa chake kwenye mchanga, hukataa kabisa kukubali kama kuna matatizo.
MBUNI



                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      

Comments

Anonymous said…
Ni kweli kabisa yaani, huku kutofahamiana tabia zetu ndio chanzo cha matatizo mengi katika jamii zetu. hahaha! mimi mwenyewe nina boss wangu huyo mtata mtupu..Duh sijui kama tutafika..

Popular posts from this blog

NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE?