Posts

Showing posts from 2017

TENDA WEMA UENDE ZAKO

Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka. Aliingia chumba cha kubadilisha Mavazi na kuvaa nguo za kazi na kuelekea    moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji. Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba Mmoja anazunguka huku na huku karibu na chumba cha upasuaji akimsubiria Daktari. Baada ya kumuona tu, Yule Baba akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?” Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze Jaziba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “ Punguza hasira?! Hivi ingekuwaje Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndie anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana. Yul...

KIJANA WA MIAKA 25

Siku Moja  kijana mwenye umri wa miaka 25 alikuwa a kichungulia nje ya dirisha la treni lililo kuwa likienda kwa kasi, akawa akisema kwa sauti ... "Baba, angalia miti in arud i nyuma! " Baba yake  alibaki  akitabasamu kwa maneno ya kijana wake … Mzee huyo hakuongea kitu bali uso wake ulionyesha maridhiyo ya maneno aliokua wakisema kija na wake. Pembeni  walimoketi palikua na wanandoa wawili. Wanadoa hao walibaki wakitazamana  kwa mshangao  juu ya  yale maneno alisema kijana  yule. Ghafla wakamsikia tena yule-kijana Akisema kwa nguvu "Baba Babaa!, angalia mawingu  yanatembea nasi!" Wanandoa wale hawakuweza kujizuia  tena kuamua kumwambia a Baba wa yule kijana, "Mzee Kwanini humpeleki Mwanao kumuona daktari?" Mzee akatabasamu na akajibu ... "Nimefanya hivyo na hivi tunatoka hospitalini, Mwanangu alikuwa haoni tangu kuzaliwa kwake, kwa mara ya kwanza leo ndio anaona." Hekima: Kila Mmoja wetu duniani ana hadithi ya maisha ...