TENDA WEMA UENDE ZAKO
Daktari
aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya
Upasuaji wa haraka. Aliingia chumba cha kubadilisha Mavazi na kuvaa nguo za kazi na
kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.
Wakati
akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba Mmoja anazunguka
huku na huku karibu na chumba cha upasuaji akimsubiria Daktari. Baada ya kumuona
tu, Yule Baba akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama
maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”
Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa
haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa
nimeshafika ningekuomba upunguze Jaziba na hasira ili nifanye shughuli yangu”
“ Punguza hasira?!
Hivi ingekuwaje Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza
kupunguza hasira? Kama mwanao ndie anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule
Baba aliongea kwa hasira sana.
Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: “ ningesema kama
vitabu vinavotuambia tuseme, “ tumeumbwa
kwa vumbi na tutaondoka kwa Vumbi, Jina la Mwenyezi Mungu Litukuzwe”. Dactari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu.
Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao
kwa Baraka za M.Mungu”
“ Kutoa Ushauri kwa
vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona Yule Baba mwenye mtoto mgonjwa.
Upasuaji ulifanyika kwa Masaa kadhaa mara tu baada ya
kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “
Asante Mungu! Mtoto wako tumeweza kumponya!”
Kama una swali lolote utamuuliza Nesi!!” Bila ya kumsikia Baba
Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
“ Kwa nini ni Mkorofi sana huyu Daktari? Yaani Hawezi hata
kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya Mwanangu” alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktari
kuondoka.
Nesi akamjibu, huku akitokwa na machozi: “ Mtoto wake alifariki jana kwenye ajari ya
gari, hivyo alikuwa katika mazishi ya Mtoto wake wakati tunampigia simu aje hospitali
kwa ajili ya Upasuaji wa Mtoto wako.
Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya Mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi
mazishi ya mtoto wake.”
Toleo la kwanza limeandikwa na ALLEGREI A. FERNANDO
HEKIMA:
“USI MUHUKUMU MTU
YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAO NA KIPI KILICHO WAKUTA KWENYE MAISHA YAO.
“ TENDA WEMA KADRI
UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO”
Comments