KIJANA WA MIAKA 25
Siku Moja kijana mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akichungulia nje ya dirisha la treni lililo kuwa likienda kwa kasi, akawa akisema kwa sauti ... "Baba, angalia miti inarudi nyuma!"
Baba yake alibaki akitabasamu kwa maneno ya kijana wake … Mzee huyo hakuongea kitu bali uso wake ulionyesha maridhiyo ya maneno aliokua wakisema kijana wake.
Pembeni walimoketi palikua na wanandoa wawili. Wanadoa hao walibaki wakitazamana kwa mshangao juu ya yale maneno alisema kijana yule.
Ghafla wakamsikia tena yule-kijana Akisema kwa nguvu
"Baba Babaa!, angalia mawingu yanatembea nasi!"
Wanandoa wale hawakuweza kujizuia tena kuamua kumwambia a Baba wa yule kijana,
"Mzee Kwanini humpeleki Mwanao kumuona daktari?" Mzee akatabasamu na akajibu ... "Nimefanya hivyo na hivi tunatoka hospitalini, Mwanangu alikuwa haoni tangu kuzaliwa kwake, kwa mara ya kwanza leo ndio anaona."
Hekima:
Kila Mmoja wetu duniani ana hadithi ya maisha yake. Usihukumu mtu kabla ya kujua Undani wa Maisha yake.
Comments