TENDA WEMA UENDE ZAKO
Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka. Aliingia chumba cha kubadilisha Mavazi na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji. Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba Mmoja anazunguka huku na huku karibu na chumba cha upasuaji akimsubiria Daktari. Baada ya kumuona tu, Yule Baba akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?” Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze Jaziba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “ Punguza hasira?! Hivi ingekuwaje Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndie anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana. Yul...