NDOTO ZA MKOSAJI
Msichana mmoja alikuwa anaelekea sokoni huku akiwa amebeba ndoo ya maziwa kichwani kwake. Akiwa anatembea alipanga mengi kichwani kwake “Nikiuza haya maziwa nitapata pesa nyingi za kununua kuku mweupe,” atanitagia mayai mengi, yatatotoa vifaranga vingi. Nitavikuza vizuri hadi vitage mayai mengi zaidi. Mayai yatakuwa mengi Zaidi na nitakuwa na kuku wengi watakao taga tena mayai na kutototoa vifaranga vingi Zaidi.. Kwa muda mfupi tu nitakuwa tajiri, nitanunua vitu vya gharama. Nitavaa nguo za ghrarama kubwa na madini kuanzia shingoni hadi miguuni mwangu. Na ikitokea siku moja niitaenda kwa Malkia, nitampelekea zawadi adimu ya thamani sana kutoka Marekani. Nitaingia kwenye Jumba lake la kifahari, mikono yangu imejaa vito vya gharama, kwa heshima nitainamisha kichwa na kumsalimu Malkia na kumwambia,…" Kabla hajasema alichotaka kumwambia Malkia, akjikuta Amedondosha ndoo aliyobeba kichwani na kumwaga maziwa yote yal...