NDOTO ZA MKOSAJI
Msichana
mmoja alikuwa anaelekea sokoni huku akiwa amebeba ndoo ya maziwa kichwani
kwake.
Akiwa
anatembea alipanga mengi kichwani kwake “Nikiuza haya
maziwa nitapata pesa nyingi za kununua kuku mweupe,” atanitagia mayai mengi, yatatotoa vifaranga
vingi. Nitavikuza vizuri hadi vitage mayai mengi zaidi. Mayai yatakuwa mengi Zaidi
na nitakuwa na kuku wengi watakao taga tena mayai na kutototoa vifaranga vingi Zaidi..
Kwa
muda mfupi tu nitakuwa tajiri, nitanunua vitu vya gharama. Nitavaa nguo za
ghrarama kubwa na madini kuanzia shingoni hadi miguuni mwangu. Na ikitokea siku moja niitaenda kwa Malkia,
nitampelekea zawadi adimu ya thamani
sana kutoka Marekani. Nitaingia kwenye
Jumba lake la kifahari, mikono yangu
imejaa vito vya gharama, kwa heshima nitainamisha kichwa na kumsalimu Malkia na
kumwambia,…"
Kabla
hajasema alichotaka kumwambia Malkia, akjikuta Amedondosha ndoo aliyobeba
kichwani na kumwaga maziwa yote
yaliyomo.
Comments