MBWA MWITU NA MBUZI
Yule
Mama mbuzi akaondoka na kuwaacha watoto wake saba wakiwa ndani ya nyumba. Baada
ya muda mfupi, wakasikia “ngo ngo ngo ngo” na sauti mlangoni ambayo inasema "Nifungulieni mlango
watoto wangu, nina zawadi kwa kila mmoja wenu". Sauti yake ilikuwa mbaya
sana na watoto wakaogopa kufungua mlango.
Mbwa mwitu akaenda kwenye soko na kuiba asali ili kuifanya sauti yake iwe nyororo. Muda mfupi baadaye, watoto wakasikia sauti nyingine mlangoni: "Nifungulieni mlango watoto wangu, mama yenu nina zawadi kwa kila mmoja wenu". Wakati huu sauti ni tamu kama ya mama yao.
Wakati wanajiandaa kufungua mlango, mtoto wa mwisho akachungulia chini ya mlango na kuona miguu mikubwa na meusi kama ya mbwa mwitu. Wakakataa kufungua mlango, na mbwa mwitu akaondoka tena.
Mbwa mwitu akaenda duka la kuandaa mikate na kuiba unga mweupe, na kisha akajipaka kwenye miguu yake yote. Akaludi tena nyumbani kwa watoto wa mbuzi na kubisha tena hodi.
“Nifungulieni mlango watoto wangu, mama yenu nina zawadi kwa kila mmoja wenu".
Watoto wakaona miguu yake meupee na kusikia sauti yake tamu, hivyo wakafungua mlango. Mbwa mwitu akaingia ndani ya nyumba na kuwachukua watoto sita. Mtoto wa mwisho akawahi kujificha nyuma ya saa kuubwa ya Babu yake, hivyo hakuweza kuchukuliwa.
Baadaye siku hiyo, mama Mbuzi anarudi kutoka msituni, akashangaa kuona mlango wa nyumba yake upo wazi na watoto wake hawaonekani isipokuwa Yule mtoto wake wa mwisho aliyejificha nyuma ya saa. Baada ya kuwatafuta kwa muda, akamuona mbwa mwitu amelala chini ya mti. Alikuwa ameshiba sana, hivyo hakuweza kutembea. Mama Mbuzi akamwita mtoto wake wa mwisho amletee Mkasi, kiwembe, Sindano na Uzi haraka sana. Akachana tumbo la Mbwa Mwitu na cha miujiza wakatoka watoto wote sita wakiwa wazima kabisaaa. Wakajaza mawe mazito tumboni kwa mbwa Mwitu na kulishona.
Wakati mbwa mwitu ana amka, akasikia kiu ya maji na kwenda mtoni kunywa maji. Alipofika Mtoni kunywa maji, akatumbukia kwenye mto na kuzamishwa kutokana na Uzito wa mawe tumboni mwake. Hivyo Wakaishi kwa amani na Furaha tele.
Asanteni:
Source: Wikipedia, the free encyclopedia (English Version)
Comments