NJIA RAHISI YA KUPATA FURAHA


Kuna siku moja Vijana 50 Walihudhuria Semina ya mafunzo ya Maisha, Baada ya mafunzo kwa njia ya majadiliano kuisha, Mwezeshaji aliwaomba viajana wafanye mafunzo kwa vitendo kwa Makundi.
Zoezi lilikuwa kama ifutavyo:
Kila kijana alipewa Puto moja, na Kuandika jina lake kwa kutumia Peni yenye Wino mzito (maker pen). Na Maputo yakakusanywa na kuwekwa kwenye Chumba kingine. 
Mwezeshaji akatoa dakika 5, vijana wote waingie kwenye chumba chenye Maputo na kutafuta puto lenye jina lake juu.
Vijana walikimbia na kuingia kwenye kile chumba, kwa fujo, vurugu, kusukumana, walitawanya Maputo, kila mmoja alikuwa akijitahidi kutafuta  jina lake.
Baada ya dakika 5 kuisha,  hakuna kijana aliyeweza kupata puto lenye jina lake.
Mwezeshaji akaludia tena zoezi kwa njia tofauti.
Akatoa Dakika 5 zingine, kila mmoja aokote Puto moja na kumpa mtu ambaye jina lake limeandikwa juu ya puto hilo.
Ndani ya dakika moja, kila mmoja alikuwa amepata puto lenye jina lake mwenyewe.
Hii inatokea katika maisha yetu. Kila Mmoja anahitaji Furaha, lakini hatujui wapi na jinsi gani tutaweza kuipata. Wakati mwingine tunatumia gharama kubwa, kuzunguka huku na kule, bila mafanikio
Mafunnzo:
Furaha na Faraja yetu zinategemea Faraja ya watu wengine. Waoneshe Faraja wengine na wao watakuludishia Faraja yako. Na hili ndilo kusudi la maisha ya mwanadamu.



Comments

Popular posts from this blog

NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE?

WANYAMA NA TABIA ZA BINADAMU