Posts

HAKUNA KAMA MAMA

Baada ya kumaliza Masomo yake, aliamua kuaga wazazi wake na kwenda Mjini kutafuta maisha. Alipofika mjini aliajiriwa kwenye kampuni ya Wachina, malipo ya mshahara wake yalikuwa madogo sana hayakuweza kukidhi mahitaji yake ya mwezi, ilikuwa ikifika katikati ya mwezi hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa inakosekana. Lakini alijitahidi kujinyima, kidogo alichokipata alikuwa akihifadhi na kila alipokuwa akiwatembelea wazazi wake alikuwa anawapelekea pesa kidogo na kuludi mjini kuendelea na maisha yake. Yule kijana alijiwekea malengo baada ya miaka mitatu aweze kuwa na mtaji wa kufanya biashara itakayo ongeza kipato   mbali na kile cha kuajiriwa.   Kila alipokuwa akimpigia simu Mama yake, cha kwanza alikuwa akiulizwa maendeleo ya mipango hiyo.   Majibu hayakuwa mazuri. Hakuna alichokuwa anakibakisha kila mwezi, ilikuwa ni ngumu kutokana maisha ya mjini, ila pamoja na hayo yote alikuwa lazima akawaone wazazi wake na kumwachia mama yake kiasi cha pesa kwa ajili ya matumizi ...

NJIA RAHISI YA KUPATA FURAHA

Kuna siku moja Vijana 50 Walihudhuria Semina ya mafunzo ya Maisha, Baada ya mafunzo kwa njia ya majadiliano kuisha, Mwezeshaji aliwaomba viajana wafanye mafunzo kwa vitendo kwa Makundi. Zoezi lilikuwa kama ifutavyo: Kila kijana alipewa Puto moja, na Kuandika jina lake kwa kutumia Peni yenye Wino mzito (maker pen). Na Maputo yakakusanywa na kuwekwa kwenye Chumba kingine.  Mwezeshaji akatoa dakika 5, vijana wote waingie kwenye chumba chenye Maputo na kutafuta puto lenye jina lake juu. Vijana walikimbia na kuingia kwenye kile chumba, kwa fujo, vurugu, kusukumana, walitawanya Maputo, kila mmoja alikuwa akijitahidi kutafuta  jina lake. Baada ya dakika 5 kuisha,  hakuna kijana aliyeweza kupata puto lenye jina lake. Mwezeshaji akaludia tena zoezi kwa njia tofauti. Akatoa Dakika 5 zingine, kila mmoja aokote Puto moja na kumpa mtu ambaye jina lake limeandikwa juu ya puto hilo. Ndani ya dakika moja, kila mmoja alikuwa amepata puto lenye jina lake mwenye...

MUONGO HAAMINIKI HATA AKISEMA UKWELI

Kulikuwa na kijana mmoja akichunga Kondoo wa kijiji juu ya kilima. Yule Kijana akajilaza juu ya kilima hiko akiwa amechoka na kuboreka   baada ya kuchunga wale kondoo kwa muda mrefu siku hiyo.  H ivyo akafikiria kufanya kitu kitakacho mchangamsha.   Akavuta pumzi   kuubwa na kupiga kelele, “Simba! Simba! Simba!   Huku akiwafukuza wale kondoo. Wanakijiji walikuja wakikimbia juu ya kilima ili kumsaidia yule kijana. Lakini walipofika juu, hawakukuta simba.   Yule kijana aliwacheka mbele ya nyuso zao zilizo jaa hasira. Wale wanakijiji wakamwambia yule kujana "Usipige kelele za Simba wakati hakuna Simba !", Wakashuka chini ya mlima huku wamekasirika. Baadaye, kijana huyo alipiga kelele za simba tena, "Simba! Simba anakimbiza kondoo!” Kwa furaha yake mbaya, aliwaangalia wanakijiji wakipanda tena kile kilima ili kumsaidia kufukuza Simba. Wanakijiji walipofika juu pasi na kuona Simba, wakasema kwa ukali, "Piga kelele za kuomba msaada wakati kuna kitu ch...

NDOTO ZA MKOSAJI

Msichana mmoja alikuwa anaelekea sokoni huku akiwa amebeba ndoo ya maziwa kichwani kwake. Akiwa   anatembea   alipanga mengi kichwani kwake “Nikiuza haya maziwa nitapata pesa nyingi za kununua kuku mweupe,”   atanitagia mayai mengi, yatatotoa vifaranga vingi. Nitavikuza vizuri hadi vitage mayai mengi zaidi. Mayai yatakuwa mengi Zaidi na nitakuwa na kuku wengi watakao taga tena mayai na kutototoa   vifaranga vingi Zaidi.. Kwa muda mfupi tu nitakuwa tajiri, nitanunua vitu vya gharama. Nitavaa nguo za ghrarama kubwa na madini kuanzia shingoni hadi miguuni mwangu.   Na ikitokea siku moja niitaenda kwa Malkia, nitampelekea zawadi   adimu ya thamani sana kutoka Marekani.   Nitaingia kwenye Jumba lake la kifahari,   mikono yangu imejaa vito vya gharama, kwa heshima nitainamisha kichwa na kumsalimu Malkia na kumwambia,…" Kabla hajasema alichotaka kumwambia Malkia, akjikuta Amedondosha ndoo aliyobeba kichwani na kumwaga   maziwa yote yal...