MZEE MWENYE HEKIMA NA BUSARA

Hapo zamani kulikuwa na Mzee mmoja mwenye busara sana, alikuwa akiishi kwenye kijiji kimoja huko nchini Korea. Aliishi maisha ya tabu sana, ambapo aliweza kujifunza sana kutokana na maisha hayo, alikuwa akitumia akili nyingi na kufikiri kwa kina sana kutatua changamoto zilizokua zikimkuta. Watu kutoka sehemu mbalimbali walimfuata na kumuomba ushauri juu ya matatizo yao. Alikuwa akisikiliza kwa umakini na unyenyekevu mkubwa sana na hata alipokuwa akitoa ushauri alikua akitoa kwa umakini na hekima pia. Hii ilifanya watu wengi zaidi kumfuata kutoka sehemu za mbali sana kuja kuwa karibu na kuzungumza nae.

Kulikuwa na Kijana mmoja pale kijijini, aliwashangaa watu wanaosafiri kwenda kuzungumza na huyo Mzee, “Anaujuzi ganu huyo mzee?” alikua akisema huyo kijana. “Hakusoma hata dirasa moja, na siamini kama anahekima kiasi gani watu wamfuate!” pindi akijiuliza kichwani kwake akapata wazo la kwenda kujaribu hiyo hekima ya yule mzee.

Yule Kijana alikwenda porini na kukamata ndege mdogo, alafu akamfunika kwa viganja vya mikono yake miwili na kwenda na kuketi chini mbele ya yule Mzee.
“Nikusaidie nini Kijana?” Yule mzee aliuliza kwa utaratibu kabisa
“Nina ndege kwenye viganja vyangu” alijibu Yule kijana.
“Unaweza kuniambia kama huyu ndege ni mzima au amekufa?” ila katika fikira zake aliwaza “kama akisema ni mzima nitamminya hadi kufa na akisema kafa, nitafungua mikono na kumuonesha kama ni mzima. Majibu yote atakayojibu nitathibitisha kuwa amekosa.”
Ila Yule mzee aliangalia kwa makini macho ya yule kijana na akamwambia, “Kijana, Maisha ya huyo ndege yapo kwenye mikono yako, ni wewe utakaye amua huyo ndege afe au abaki kuishi kwa furaha na amani”

Comments

Anonymous said…
Lucky Club: The Best Casinos of 2021 - Lucky Club Live
Our Top Five · 1. luckyclub.live The Largest Selection · 2. Lucky Club - The World's First Online Casino · 3. The Best Online Casino · 4. The Best Online

Popular posts from this blog

NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE?

WANYAMA NA TABIA ZA BINADAMU