Posts

Showing posts from 2018

NJIA RAHISI YA KUPATA FURAHA

Kuna siku moja Vijana 50 Walihudhuria Semina ya mafunzo ya Maisha, Baada ya mafunzo kwa njia ya majadiliano kuisha, Mwezeshaji aliwaomba viajana wafanye mafunzo kwa vitendo kwa Makundi. Zoezi lilikuwa kama ifutavyo: Kila kijana alipewa Puto moja, na Kuandika jina lake kwa kutumia Peni yenye Wino mzito (maker pen). Na Maputo yakakusanywa na kuwekwa kwenye Chumba kingine.  Mwezeshaji akatoa dakika 5, vijana wote waingie kwenye chumba chenye Maputo na kutafuta puto lenye jina lake juu. Vijana walikimbia na kuingia kwenye kile chumba, kwa fujo, vurugu, kusukumana, walitawanya Maputo, kila mmoja alikuwa akijitahidi kutafuta  jina lake. Baada ya dakika 5 kuisha,  hakuna kijana aliyeweza kupata puto lenye jina lake. Mwezeshaji akaludia tena zoezi kwa njia tofauti. Akatoa Dakika 5 zingine, kila mmoja aokote Puto moja na kumpa mtu ambaye jina lake limeandikwa juu ya puto hilo. Ndani ya dakika moja, kila mmoja alikuwa amepata puto lenye jina lake mwenye...

MUONGO HAAMINIKI HATA AKISEMA UKWELI

Kulikuwa na kijana mmoja akichunga Kondoo wa kijiji juu ya kilima. Yule Kijana akajilaza juu ya kilima hiko akiwa amechoka na kuboreka   baada ya kuchunga wale kondoo kwa muda mrefu siku hiyo.  H ivyo akafikiria kufanya kitu kitakacho mchangamsha.   Akavuta pumzi   kuubwa na kupiga kelele, “Simba! Simba! Simba!   Huku akiwafukuza wale kondoo. Wanakijiji walikuja wakikimbia juu ya kilima ili kumsaidia yule kijana. Lakini walipofika juu, hawakukuta simba.   Yule kijana aliwacheka mbele ya nyuso zao zilizo jaa hasira. Wale wanakijiji wakamwambia yule kujana "Usipige kelele za Simba wakati hakuna Simba !", Wakashuka chini ya mlima huku wamekasirika. Baadaye, kijana huyo alipiga kelele za simba tena, "Simba! Simba anakimbiza kondoo!” Kwa furaha yake mbaya, aliwaangalia wanakijiji wakipanda tena kile kilima ili kumsaidia kufukuza Simba. Wanakijiji walipofika juu pasi na kuona Simba, wakasema kwa ukali, "Piga kelele za kuomba msaada wakati kuna kitu ch...

NDOTO ZA MKOSAJI

Msichana mmoja alikuwa anaelekea sokoni huku akiwa amebeba ndoo ya maziwa kichwani kwake. Akiwa   anatembea   alipanga mengi kichwani kwake “Nikiuza haya maziwa nitapata pesa nyingi za kununua kuku mweupe,”   atanitagia mayai mengi, yatatotoa vifaranga vingi. Nitavikuza vizuri hadi vitage mayai mengi zaidi. Mayai yatakuwa mengi Zaidi na nitakuwa na kuku wengi watakao taga tena mayai na kutototoa   vifaranga vingi Zaidi.. Kwa muda mfupi tu nitakuwa tajiri, nitanunua vitu vya gharama. Nitavaa nguo za ghrarama kubwa na madini kuanzia shingoni hadi miguuni mwangu.   Na ikitokea siku moja niitaenda kwa Malkia, nitampelekea zawadi   adimu ya thamani sana kutoka Marekani.   Nitaingia kwenye Jumba lake la kifahari,   mikono yangu imejaa vito vya gharama, kwa heshima nitainamisha kichwa na kumsalimu Malkia na kumwambia,…" Kabla hajasema alichotaka kumwambia Malkia, akjikuta Amedondosha ndoo aliyobeba kichwani na kumwaga   maziwa yote yal...

MBWA MWITU NA MBUZI

Image
Kulikuwa na Mbuzi  Mmoja na Watoto wake saba. Siku moja alienda Msituni kutafuta chakula na kuwaacha watoto wake nyumbani. Lakini Kabla ya kuondoka, akawaonya watoto wake kuhusu “Mbweha” kwamba, kuna Mbweha Mkubwa Hatari sana, atakuja na kujaribu kuingia ndani ya nyumba na Kuwatafuna. Mbwa mwitu atajifanya kuwa mama yenu na kuwashawishi kufungua mlango. Watoto wa Mbuzi wataweza kumtambua mama yao wa kweli kwa miguu yake meupe na sauti nzuri na nyororo.  Yule Mama mbuzi akaondoka na kuwaacha watoto wake saba wakiwa ndani ya nyumba. Baada ya muda mfupi, wakasikia “ngo ngo ngo ngo” na sauti mlangoni   ambayo inasema "Nifungulieni mlango watoto wangu, nina zawadi kwa kila mmoja wenu". Sauti yake ilikuwa mbaya sana na watoto wakaogopa kufungua mlango. Mbwa mwitu akaenda kwenye soko na kuiba asali ili kuifanya sauti yake iwe nyororo. Muda mfupi baadaye, watoto wakasikia sauti nyingine mlangoni: "Nifungulieni mlango watoto wangu, mama yenu nina zawadi kwa kila ...